Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Palestina yapendekeza kuboreshwe mashirikiano ya kitaalumu baina yake ya UNCTAD

Palestina yapendekeza kuboreshwe mashirikiano ya kitaalumu baina yake ya UNCTAD

Mawaziri wa Kipalestina pamoja na maafisa wenginewa ngazi za juu wamesifu na kupongeza juhudi zinaazoendelea kuchukuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa UNCTAD linalochukua shabaha ya kusukuma mbele shughuli za kimaendeleo hasa katika eneo ka ukusaji uchumi.

Hivi karibuni ujumbe wa UNCTAD ilifanya ziara ya siku tano nchini humo ukilenga kuimarisha mashirikiano ya kiutendaji lakini pamoja na kuboresha mashirikiano ya kiufundi baina ya sehemu zote mbili.

Palestina pamoja na kusifu mashiriano hayo ya kubadilishana ujuzi lakini imeelezea pia haja ya kuendelea kuboresha mashirikiano hayo ili kuzaa matunda mema kwa wakati muafaka.

Katika ziara yake hiyo mratibu wa UNACTAD Mahmoud Elkhafif aliyeambatana na mchumi Randa Jamal walikutana na kufanya mazungumzo na maafisa mbalimbali ikiwemo waziri wa uchumi Dr Jawad Naji na mwenzake wa fedha Dr nabil Kassis