Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza Ubaguzi wa Rangi yahitimisha Tathmini ya ripoti ya Ecuador

8 Agosti 2012

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na utokomezaji wa ubaguzi wa rangi Jumatano imehitimisha tathimini ya ripoti ya Ecuador kuhusu utekelezaji wa mkataba wa kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi wa rangi katika taifa hilo.

Waziri wa utamaduni wa Ecuador Maria Fernanda Espinosa akiwasilisha ripoti hiyo kwenye baraza la haki za binadamu amesema ni kwa njia tuu ya kuweka sheria kali za kulinda haki za binadamu ndipo taifa hilo litafanikiwa kuwa la kidemokrasia na kuhakikisha wanaume a wanawake wote wanakuwa na hali sawa.

Amesema mwaka 2008 Ecuador ilipitisha katiba mpya ambayo inachagiza maisha bora kwa wote ikijumuisha haki ya kuwa na maji, elimu, malazi, makazi,afya, ajira na ustawi wa jamii na wamepiga hatua kubwa katika kupambana na umasikini na kwamba taifa hilo linaelekea kutokomeza mifumo yote ya ubaguzi wa rangi.

Kamati inatarajiwa kutoa tathimini ya mwisho na mapendekezo yake kuhusu ripoti ya Ecuador mwishoni mwa kikao cha kamati kitakacho kamilika Agosti 31 mwaka huu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter