IOM yaendelea kuwasaidia raia wa Syria wanaokimbia na kuingia nchini Iraq

31 Julai 2012

Tangu kufunguliwa kwa mipaka ya Iraq kwa wakimbizi kutoka Syria tarehe 24 mwezi Julai mwaka huu zaidi ya watu 2800 wamevuka mpaka na kuingia nchini Iraq. Huku tayari wakimbizi 8500 wakiwa wamepiga kambi kaskazini mwa Iraq kwenye eneo la Kurdistan ina maana kwamba kwa sasa jumla ya wakimbizi 11,000 kutoka Syria wako nchini Iraq.

Kando na wakimbizi hao kutoka Syria wanaoingia nchini Iraq raia 18,000 wamerejea nchini mwao kutoka mji wa Aleppo ulio nchini Syria siku za hivi karibuni baada ya mji huo kukumbwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi. Kati ya sababu walizotaja zilizochangia wao kuhama Syria ni pamoja mauaji ya kiholela pamoja na oporaji, uhaba wa chakula , maji na huduma za afya na hofu ya mzozo huo kuendelea kuwa mbaya. Jumbe omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud