Ban Awataka Viongozi wa Rwanda na DRC Kukutana ili Kuzikabili Hujuma za Waasi wa M23

12 Julai 2012

Huku akiwatolea mwito viongozi wa mataifa ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameweka wasiwasi wake juu ya kuendelea kuimarika kwa vikosi vya waasi vinavyoendesha machafuko mashariki mwa DRC.

Kundi hilo la waasi lililojipachika jina la M23 ni muunganiko wa vikosi kadhaa ambavyo hapo awali vilikuwa sehemu ya jeshi la taifa lakini ilipofika mwezi April vilikimbilia msituni na kuanzisha uasi.

Likiwa chini ya Bosco Ntaganda anayesakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kundi hilo linadaiwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kusabisha watu kadhaa kupoteza maisha.

Akitizama mkwamo huo wa mambo, Katibu Mkuu Ban amewatolea mwito rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na yule wa DRC Joseph Kabila kufanya mazungumzo kuhusu kuzorota kwa hali hiyo ya usalama ambayo inasababisha mamia ya raia kuingia kwenye mahangaiko.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter