MONUSCO yatilia shaka Mwenendo wa Askari Waasi mashariki mwa DRC

10 Julai 2012

Vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC, imesema inatiwa wasiwasi na hali ya mambo inayoendelea kujiri sasa huko mashariki mwa taifa ambako vikosi vya waasi m23 vinaendesha mashambulizi na uvamizi wa raia.

Msemaji wa vikosi hivyo MONUSCO amesema makundi hayo ya waasi yanaripotiwa kupiga hatua kusonga mbele kwa kutwaa maeneo muhimu jambo ambalo linazidisha hali ya wasiwasi.

Hata hivyo vikosi hivyo vya kimataifa kwa kushirikiana na vikosi vya serikali vimeanzisha jitihada za kukabiliana na waasi hao kwa kuweka nguvu ya pamoja. Kundi hilo la M23ambalo linaongozwa na kiongozi muasu  Bosco Ntaganda wanasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kutokana na hujuma wanazoendesha katika maeneo ya raia

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter