Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muda muafaka wa kufuatilia Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Silaha:Ban

Ni muda muafaka wa kufuatilia Mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Silaha:Ban

Mkutano kuhusu mkataba wa kimataifa wa biashara ya silaha umeanza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwa mara ya kwanza nchi wanachama wamekusanyika kujadili mkataba utakaokuwa ukifuatilia utaratibu wa kimataifa wa biashara ya silaha. Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kila aliyehudhuria mkutano huo anaandika historia, kwani ni muhimu na inatia moyo.

Ameongeza kuwa huu ni wakati muafaka wa kujadili mada hii, kwani kuna hatua zilizopigwa kuhusu suala la silaha za maangamizi lakini jumuiya ya kimataifa haikuwa na kasi inayostahili kuhusu kawaida ya biashara ya silaha na hakuna mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na upeo wa biashara ya silaha duniani. Amesema suala hili linasikitisha na ufuatiliaji dunia wa kimataifa wa biashara ya silaha unachochea vita vya wenyewe kwa wenyewe, usalama mdogo na kuyapa uwezo makundi ya kigaidi na mitandao ya uhalifu.