Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya Umma ya Ulaya imo Hatarini:ILO

Sekta ya Umma ya Ulaya imo Hatarini:ILO

Uchunguzi mpya wa Shirika la Ajira duniani, ILO umebainisha kuwa uhaba wa fedha umesababisha kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha katika sekta ya umma, kupungua kwa nafasi za ajira pamoja na mishahara. Ripoti ya uchunguzi huo pia inataja umuhimu wa mazungumzo ya kijamii kati ya serikali na wafanyikazi katika muktadha huo wa kiuchumi.

Uchunguzi huo ulihusu mabadiliko katika sekta ya umma Ulaya, ukiangazia kiwango cha mabadiliko hayo, athari zake, pamoja na masuala ya kisera. Ripoti inaonyesha shinikizo la dharura la kubadilisha matumizi ya fedha za serikali mara nyingi hupendelea mambo kama kupunguza matumizi, kupunguza nafasi za ajira na mishahara katika sekta ya umma. Alice Kariki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)