Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar na UM Wasaini Mpango wa Kuwaachilia Askari Watoto:UNICEF

Myanmar na UM Wasaini Mpango wa Kuwaachilia Askari Watoto:UNICEF

Serikali ya Myanmar na Umoja wa Mataifa leo wametia sainiampango wa kuchukua hatua ya kuzuia uingizaji na utumiaji wa watoto katika majeshi ya Myanmar Tatmadaw na kuruhusu kuachiliwa kwa askari watoto.

Mpango huo umetiwa saini mjini Na Pyi Taw kati ya meja jenerali Ngwe Thein mkurugenzi wa wizara ya ulinzi, meja jeneral Tin Maung Win makamu mkuu wa majeshi ya Myanmar, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Ashok Nigan na mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ramesh Shrestha. Tiwaji saini huo umeshuhudiwa pia na mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya watoto kwenye mvita vya silaha Radhika Coomaraswamy. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)