Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha Kamati ya Urithi wa Dunia chaanza kujadili Maendeleo endelevu

Kikao cha Kamati ya Urithi wa Dunia chaanza kujadili Maendeleo endelevu

Kikao chja 36 cha kamati ya kimataifa ya urithi wa dunia kimeanza huku shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO likiadhimisha mwaka wa 40 tangu kupitishwa mkatana wa urithi wa dunia.

Kikao hicho cha kamati kimeanza Jumapili St Petersburg kukiwa na changamoto nyingi zinazokabili uhifadhi wa urithi wa dunia huku mada kuu inayojadiliwa ni maendeleo endelevu. Akizungumza katika mkutano huo ut5akaokamilika Julai 6, mwenyekiti wa kamati ya urithi wa dunia Elenora Valentinovna Mitrofanova amewataka washiriki kuzingatia umuhimu wa urithi wa dunia, akisema ni lazima kutafakari ukweli ulio bayana kwamba maeneo ya urithi wa dunia yanakwenda sambamba na mila, desturi, uzoefu na la msingi zaidi juhudi za jamii husika. Kwa kifupi amesema wazawa na watu wa asili ni nguzo muhimu katika uhifadhi wa urithi wa dunia. Naye mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema kuna changamoto na shinikizo kubwa katika kuhifadhi urithi wa dunia hivi sasa kuliko siku za nyuma. Ametaka wadau wote kwa msitari wa mbele kuhakikisha vizazi vijavyo havikosi kumbukumbu ya mila na desturi zao.