Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amlilia aliyekuwa rafiki wa UM Dr. J. Michael Adams

Ban amlilia aliyekuwa rafiki wa UM Dr. J. Michael Adams

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa chama cha kimataifa cha vyuo vikuu, Dr J. Michael Adams aliefariki dunia leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na maradhi.

Katika salamu zake, Ban amemwelezea rais huyo kuwa pamoja na majukumu yake ya kitaalamu lakini alikuwa rafiki mwema wa Umoja wa Mataifa na kwa maisha yake binasfi. Dr Adams ambaye pia alipata kuwa rais wa chuo kikuu Fairleigh Dickinson cha New Jersey,atakumbukwa kutokana na mchango wake mkubwa katika uwanja wa ujenzi wa demokrasia,haki za binadamu na mafungamano ya kikanda.

Ban ameelezea namna dunia itavyomkosa mwanataalamu huyo mashuhuri ambaye pia anatajwa kushiriki katika majukumu kadhaa ya kimataifa.