Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadilia changamoto zinazowaandama walinzi wa amani

Baraza la Usalama lajadilia changamoto zinazowaandama walinzi wa amani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadilia hali ngumu zinazowandama vikosi vya kimataifa vinavyoendesha operesheni za amani kote duniani.  Baraza hilo limetambua ugumu na vikwazo vinavyowaandama wafanyakazi hao wa kimataifa pindi wawapo kwenye maeneo ya kazi ikiwemo utekelezaji wa miongozo ya utanzuaji mizozo na ulinzi wa amani.

 Umoja wa Mataifa unajumla ya wafanyakazi 120,000 ambao wamegawanyika kwenye maeneo ya kijeshi, polisi na wafanyakazi wa kawaida ambao wametawanyika duniani kote wakiendesha operesheni za ulinzi wa amani.

 Hata hivyo vikosi hivyo vya ulinzi wa amani bado vinaandamwa na changamoto chungu nzima ikiwemo zile zinazotishia uhai wa maisha yao.