Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwigizaji Ed Norton atetea bayo-annuai kwenye mkutano wa Rio+20

Mwigizaji Ed Norton atetea bayo-annuai kwenye mkutano wa Rio+20

Mwigizaji filamu, Ed Norton yupo kwenye mkutano wa Rio+20 ili kuchagiza uzingatiaji wa aina za viumbe wanaoangamia. 

Norton, ambaye ni nyota wa filamu kama ‘Fight Club’ na ‘The Incredible Hulk,’ amekuwa balozi mwema wa shirikisho la Umoja wa Mataifa kuhusu bio anuai, yaani CBD tangu mwaka 2010.

Kwenye mkutano wa Rio+20, nyota huyo anatarajiwa kuisaidia CBD kuzipigia debe kanuni za ulinzi wa mazingira na mali ya asili. Ametoa pia zawadi kwa washindi wa tuzo ya Equator kutoka kote ulimwenguni Jumatao jioni. Ed Norton anasema ingawa huenda ni vigumu kuelewa bio anuai, inagusa maisha ya watu kwa njia kadha wa kadha: tokea upataji maji safi, hadi matumizi ya mimea kutengeza dawa.

(SAUTI YA ED NORTON)