Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasambaza misaada nchini Myanmar

UNHCR yasambaza misaada nchini Myanmar

Bado hali kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar inabaki kuwa tete kutokana na ghasia ambazo zimeshuhudiwa siku 10 zilizopita. Kulingana na makadirio ya serikali karibu watu 48,000 wamelazimika kuhama makwao kufuatia ghasia zilizoanza kushuhudiwa juma lililopita.

Kufuatia ombi la msaada lililotolewa na serikali ya Myanmar kwa Umoja wa Mataifa, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR litatoa mahitaji muhimu kama makao, mablanketi pamoja na mito ya kulalia kwa watu hao.

 Wakati huo huo Shirika la mpango wa Chakula Dunian WFP limeongeza usambazaji wake wa chakula kwa maelfu ya watu waliohama makwao kutoakana na ghasia kwenye jimbo la Rakhine Kaskazini.