Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakaribisha mazungumzo kati ya Sudan na Sudan Kusini

Baraza la Usalama lakaribisha mazungumzo kati ya Sudan na Sudan Kusini

Wanachama wa Baraza la Usalama la UM wamekaribisha kurejelea kwa mazungunmzo kati ya Sudan na Sudan Kusini chini ya tume maalum ya Muungano wa Afrika. Katika taarifa ilotolewa baada ya mkutano wake wa Jumatatu, wanachama wa Baraza la Usalama wamesema kuwa ghasia zimepunguzwa kwenye maeneo ya mpakani, na kupongeza pande zote mbili kwa hatua zilizopigwa katika kutekeleza azimio nambari 2046 la Baraza hilo.

Hata hivyo, wanachama hao wa Baraza la Usalama wameelezea wasiwasi wao kuhusu chelewa chelewa, na kusisitiza kwamba sehemu muhimu za azimio hilo bado hazijatafutiwa suluhu na pande zote mbili. Wameongeza kwamba Sudan na Sudan ya Kusini hazina budi kupata suluhu kwa masuala yaliyosalia katika muda uliowekwa na maelekezo ya Muungano wa Afrika na Azimio namba 2046.