Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ahofia ukiukaji zaidi wa haki za binadam DRC

Pillay ahofia ukiukaji zaidi wa haki za binadam DRC

Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamewalazimu maelfu ya watu kuhama makwao, amesema leo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadam katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, katika ripoti yake mpya.

Bi Pillay ameelezea hofu yake kuwa uhalifu zaidi dhidi ya raia huenda ukatendeka katika eneo hilo na wasiwasi wake kuhusu usalama wa wakazi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Mapigano bado yanaendelea kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23, ambao wamejiondoa katika jeshi la taifa, chini ya uongozi wa kundi la watu wanaojulikana vyema hasa kwa ukiukaji wa haki za binadam uliokithiri nchini humo na hata kote duniani. Rupert Colville ni msemaji wa afisi ya Kamishna Pillay

[CLIP YA RUPERT COLVILLE]