Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza haja ya kuhifadhi udongo kwa maendeleo ya binadamu

Ban asisitiza haja ya kuhifadhi udongo kwa maendeleo ya binadamu

 

Katibu Mkuu Umoja wa MataifaBan Ki-moon ametoa mwito akitaka kuweko kwa mikakati madhubuti ili kuhifadhi udongo ambao ndiyo tegemeo kuu la maisha ya binadamu.

Ban amesisitiza kuwa kunapaswasasa kuchukuliwa hatua za haraka kurejesha kwenye ubora wake udongo huoambao kwa kiwango kikubwa umekubwa na uharibifu.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kuadhimisha siku ya kimataifa ya kukabiliana na hali iletayo jangwa,Ban amesema kuwa dunia bila udongo wenye rutuba haiwezi kusonga mbele.

Kwa hivi sasa dunia inajiaandaana mkutano wa kimataifa wa maendeleo endelevu unaotazamiwa kufanyika kuanziaJune 20 -22 huko Rio de Janeiro.Zaidi ya wakuu wa nchi 100 pamoja na wageniwengine mashuhuri wanatarajia kuhudhuria kwenye mkutano nhuo unaojulikana“Rio+20”