Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahuzunishwa na kifo cha prince Nayef wa Sauddi Arabia

Ban ahuzunishwa na kifo cha prince Nayef wa Sauddi Arabia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea husuni yake kutokana na kifo cha mwana wa kifalme Nayef bin Abdulaziz al-Saud ambaye pia alikuwa ni waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani nchini Saudi Arabia.

Kwenye taarifa kupitia kwa msemaji wake Ban amasema

kuwa Prince Nayef alijitolea kuhakikisha kuwepo usalama nchini Saudi Arabia akiongeza kuwa pia alichangia kubuniwa kwa kituo cha kupambana na ugaidi nchini Saudi Arabia.

Kituo hicho kilibuniwa mwezi Septemba mwaka 2010 kupitia usaidizi wa serikali ya Saudi Arabia na kina jukumu la kusaidia mikakakati ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi iliyotekelezwa na Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa mwaka 2006.