Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wanne wa ICC wanashikiliwa Libya

Maafisa wanne wa ICC wanashikiliwa Libya

Maafisa wanne wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kiivita ICC wanashikiliwa nchini Libya katika kipindi cha wiki moja sasa na tayari rais wa mahakama hiyo Jaji Sang-Hyun Song, ametoa mwito akitaka waachie huru mara moja.

Maafisa hao waliwekwa kizuizini kuanzia June 7 mwaka huu wakati walipokuwa kwenye ziara ya ujumbe maalumu nchini humo. Pamoja na kuwa na kinga za kidiplomasia hata hivyo mamlaka nchini humo ziliwakamata na kuwaweka kizuizini.

Akijadilia suala hilo, rais huyo wa ICC amesema kuwa lazima watumishi hao waachie tena bila vikwazo vyovyote.

ICC imesema kuwa inaendelea kuwasiliana na mamlaka za Libya ili kujiridhisha na usalama wa watumishi hao na wakati huo huo akitaka waachiwe mara moja