Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukaji wa Haki za Binadamu bado unaendelea Syria:UM

Ukiukaji wa Haki za Binadamu bado unaendelea Syria:UM

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa umebainisha kuwa vikosi vya usalama vya Syria pamoja na wapiganaji wa upinzani wanakiuka haki za binadamu kupindukia, licha ya usitishaji mapigano kutangazwa wiki sita zilizopita.

Katika ripoti ambayo imetolewa leo, wanajeshi na vikosi vya usalama vya serikali vilifanya ukiukaji mkubwa zaidi, ukiwemo kurusha mabomu kwenye makazi ya raia na mauaji ya watu walokamatwa.

Ripoti hiyo, ambayo imetokana na uchunguzi ulofanywa tangu mwezi Machi, inasema waasi wenye silaha pia waliwatesa na kuwaua wanajeshi walokamatwa na wafuasi wa serikali, pamoja na kuwateka nyara raia.