Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liechtenstein imetoa dola 100,000 kwa URWA kusaidia wakimbizi wa Palestina

Liechtenstein imetoa dola 100,000 kwa URWA kusaidia wakimbizi wa Palestina

Liechtenstein imetangaza Jumatatu kwamba itachangia dola za Kimarekani 109,231 kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Akizungumzia msaada huo kamishina wa UNRWA Filippo Grand anashukuru sana kwa mchango huo ambao utasaidia bajeti yao, na hususani katika kipindi hiki kigumu chenye changamoto za kichumi. Naye Martin Frick mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya nje ya Liechenstein amesema nchi yake imejidhatiti kuendelea kutoa msaada kwa kazi za UNRWA, kuwalinda wakimbizi wa Kipalestina na kuhakikisha suluhu ya matatizo yao inapatikana.