Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya majadiliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa

Ban afanya majadiliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na majadiliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius kuhusu siasa za kimataifa bila kuweka kando mkwamo wa amani unaoshuhudiwa huko Syria.

Katika mkutano wao huo viongozi hao wameijadilia hali ilivyo katika nchi za Lebanon, Guinea-Bissau, Mali na eneo la Sahel maeneo ambayo katika siku za hivi karibi yamepamba katika ukurasa wa kimataifa.

Ama viongozi hao waliokutana mjini New York wamejadilia pia sokomoko la usakaji amani huko Mashariki ya Kati pamoja na mkutano ujao wa kimataifa wa maendeleo endelevu ujulikanao Rio +20 utakaofanyika mwezi ujao huko Rio de Janeiro, Brazil