Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kofi Annan alaani vikali shambulio la bomu lililokatili maisha Damascus

Kofi Annan alaani vikali shambulio la bomu lililokatili maisha Damascus

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amelaani vikali shambulio la bomu lililofanyika mapema Alhamisi mjini Damascus Syria.

Annan ameshitushwa na maisha ya watu yaliyopotea kufuatia milipuko miwili na ametuma salamu za rambirambi ya familia ya waliokufa na kujeruhiwa.

Watu zaidi ya 40 wamekfa na wengine wengi kujeruhiwa katika tukio hilo. Annan amesema vitendo hivyo havikubaliki na ni lazima visitishwe mara moja. Ahmed Fawzi ni msemaji wa Kofi Annan.

(SAUTI YA AHMED FAWZI)

Mgogoro wa Syria ulianza Machi 2011 wakati waandamanaji walipomiminika mitaani kama ilivyokuwa maeneo mengine ya Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. Hadi sasa watu 9000 wamepoteza maisha wengi kujeruhiwa na maelfu kuyakimbia makazi yao.