Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan kuwasafirisha nyumbani raia wa Sudan Kusini

Sudan kuwasafirisha nyumbani raia wa Sudan Kusini

Serikali ya Sudan imebadili uamuzi wa awali wa kuwafukuza takriban raia 15,000 wa Sudan Kusini waliokwama kwenye mji wa Kosti ulio umbali wa kilomita 200 kusini mwa mji mkuu Khartoum. Raia hao wa Sudan Kusini ambao wamesubiri kwa miezi kadhaa kusafirishwa kwenda nchini mwao walikuwa wameamrishwa kuondoka kwenye mji huo tarehe tano mwezi huu.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa serikali ya Sudan sasa imejitolea kuwasafirisha watu hao kwa njia ya ndege kutoka mjini Khartoum kwenda mji mkuu wa Sudan Kusini Juba. Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anasema kuwa hata kama shughuli hiyo itachukua majuma kadha kukamilika ndiyo njia bora ya kusafirisha raia hao wa Sudan Kusini kwa usalama.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)