Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hugh Masekela aelezea umuhimu wa Jazz duniani

Hugh Masekela aelezea umuhimu wa Jazz duniani

Mwanamuziki mkongwe na mpiga trumpet mashuhuri kutoka Afrika ya Kusini Hugh Masekela na wanamuziki wengine wa Jazz wamefanya maandalizi ya kutosha siku ya Jumapili wakijiandaa kwa maadhimisho ya kwanza ya kimataifa ya siku ya Jazz.

Siku hiyo ya kimataifa ilipitishwa na UNESCO mwaka 2011 na shirika hilo linasema lengo la siku ya Jazz ni kuelimisha kuhusu umuhimu wa Jazz kama nyenzo ya kuelimisha na kuchagiza amani, umoja, majadiliano na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa watu. Akizungumza na Rasio hii ya Umoja wa Mataifa mwanamuziki Hugh Masekela anasema mziki wa Jazz umekuwa na athari na ushawishi mkubwa

(SAUTI YA HUGH MASEKELA)