Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya UM ya Haki za Binadamu yalaani mauaji ya mwandishi habari Brazil

Ofisi ya UM ya Haki za Binadamu yalaani mauaji ya mwandishi habari Brazil

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR imelaani mauaji ya mwandishi wa habari kutoka Brazil.

Decio Sa, mwandishi wa habari aliyekuwa anaripoti kuhusu masuala ya siasa, rushwa na uhalifu alipigwa risasi alipokuwa katika bar moja mji wa Sao Luis, tarehe 23 Aprili.

Msemaji wa OHCHR Rupert Colville amesema Ofisi hiyo imeshangazwa na mauaji hayo ambayo yamejumuisha idadi ya waandishi habari waliouawa nchini Brazil mwaka huu kufikia wanne.

"Tunalaani mauaji yake na tunatiwa wasiwasi na kile kinachoonekana kuwa tabia ya kuwaua waandishi wa habari na tabia hii inadhoofisha uhuru wa kujieleza nchini Brazil. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiona haja ya watetezi wa Brazil wa haki za binadamu, ikiwemo waandishi wa habari, kuwa na uwezo wa kufanya kazi yao bila hofu ya vitisho au matokeo mabaya zaidi. Tunakaribisha hatua ya mamlaka ya taifa hilo kuwa na nia ya kufanya uchunguzi wa kina na tunatoa wito kwa kesi hii na kesi nyingine zilizo sawa kupewa kipaumbele ili wahusika wasitiwe nguvu kutokana na ukosefu uliopo wa uwajibikaji.