Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rio+20 ni fursa nzuri ya kuweka ajenda mpya ya maendeleo:UNESCO

Rio+20 ni fursa nzuri ya kuweka ajenda mpya ya maendeleo:UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limesema mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu mwaka 2012 au Rio+20 ni fursa nzuri ya kuweka ajenda mpya kwa ajili ya mustakhbali endelevu wa baadaye.

Wakati wajumbe wanakutana New York kwa ajili ya duru ya pili ya majadiliano yasiyo rasmi kuhusu mswaada wa matokeo ya mkutano wa Rio +20, kumeandaliwa tukio maalumu la kuwafahamisha kuhusu thamani ya kulinda mazingira ya pwani kwa kupitia mpango maalumu uitwao blue carbon kama njia ya kuhakikisha ulinzi wa maeneo ya pwani na maendeleo yanayojali mazingira kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa.

UNESCO inasema hudma zinazotolewa na mazingira ya pwani na makazi ya viumbe vya majini ni muhimu sana kwa chakula, usalama na kutokomeza umasikini pamoja na kukuza uchumi wa mataifa yanayotegemea mazingira ya pwani.