Wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wataka kutambuliwa katika katiba mpya Tanzania

16 Aprili 2012

Umoja wa Mataifa, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na wanaharakati mbalimbali wa kupigania haki ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wameendelea kupaza sauti wakizitaka serikali duniani kutambua na kuheshimu haki za wanawake na wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanawake, au mashoga.

Mkusuko huo umeyachagiza makundi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Tanzania kujitokeza na kutaka kupewa nafasi katika katiba mpya. Hivi sasa taifa hilo la Afrika ya Mashariki lipo katika harakati ya kukusanya maoni kuhusu kuandikwa kwa katiba mpya. Mengi zaidi na mwandishi wetu wa Dar es salaam George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)