Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua utoaji wa damu kwenye jimbo la Darfur

UM wazindua utoaji wa damu kwenye jimbo la Darfur

Asilimia 25 ya vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua kenye jimbo la Darfur huwa vinachangiwa na kupoteza kiasi kikubwa cha damu na ukosefu wa damu ya ziada. Kutokana na hilo kundi la Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur limezindua kampeni ya kutoa damu kote kwenye jimbo la Darfur kama moja ya njia ya kutafuta suluhu na tatizo hili.

Hatua hii inajiri wakati ambapo wizara ya afya kwenye jimbo la Darfur inapoandaa sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa kuhusu uzazi ulio salama. Lengo la sherehe hizo ni kuweka jitihada zaidi na kutoa uwezo katika kufikia suala la uzazi ulio salama.