Waathiriwa wa majaribio ya mitambo ya nyuklia Marshall bado wanateseka:UM

30 Machi 2012

Mtaalamu mmoja kutoka Umoja wa Mataifa ameonya kuwa jamii za watu walioathiriwa na jaribio la mitambo ya kinyuklia miaka sitini iliyopita katika kisiwa cha Marshall bado wanaandamwa na jinamizi la upweke.

Calin Georgescu amezitaka nchi mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani na jumuiya za kimataifa kutafuta njia mujaribu kushughulikia kadhia inayowaandama wananchi hao.

Ameeleza kuwa jamii kubwa ya watu kwenye eneo hilo wanasalia kuwa ni watu wenye mashaka na hofu huku wakiendelea kuishi maisha ya kuhama hama katika nchi yao wenyewe.

Amesema baadhi yao  ni waathirika wa muda mrefu wa afya wakati wengine wakikosa matumaini ya kufungamana na upande mwingine wa jamii.

Hayo yamejiri baada ya mtaalamu huyo kufanya ziara maalumu kwa ajili ya kukusanya taarifa za kujiridhisha kuhusiana na hali jumla ya maisha kwenye kisiwa hicho.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter