Skip to main content

IAEA yatoa ripoti kuhusu mipango mipya ya usalama wa nyuklia nchini Japan

IAEA yatoa ripoti kuhusu mipango mipya ya usalama wa nyuklia nchini Japan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA limewasilisha ripoti yake kuhusu uchunguzi lililoendesha kuhusu usalama wa mipango ya nyuklia wa taifa la Japan baada taifa hilo kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi ambapo kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi kiliharibiwa.

Uchunguzi huo ulifanywa na kundi la wataalamu kutoka shirika la IAEA walioizuru nchi hiyo mwezi Januari kwa mwaliko wa serikali ya Japan.

Mwezi Machi mwaka 2011 kinu cha Fukushima Daichi kiliharibiwa na tetemeko kubwa la ardhi pamoja na gharika ya tsunami.

Tetemeko hilo la ardhi lilisababisha kulipuka kwa kinu hicho ajali iliyotajwa kuwa mbaya zaidi kuwai kutokea tangu  kutokea kwa ajali ya Chernobyl  mwaka 1986.