Ban ahudhuria mkutano wa usalama wa nyuklia DPRK

26 Machi 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anakutana na viongozi mbalimbali wa dunia katika mkutano wa siku mbili kuhusu usalama wa nyuklia unaofanyika Korea Kusini.

Zaidi ya wakuu wa nchi 50 na mashirika ya kimataifa wamekusanyika Seoul kujadili njia za kukabiliana na tishio la ugaidi wa nyuklia pamoja na kulinda vifaa, zana na mitambo ya nyuklia.

Eduardo del Buey ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA EDUARDO DEL BUEY)

Ban amerejea wito wake kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK kutekeleza maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Korea ya Kaskazini imetangaza hivi karibuni kwamba itatuma satellite mwezi April katika kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim Il-sung.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter