Ofisi ya UM yaonya kuwa hakutakuwa na ulipizaji kizazi dhidi ya watetea haki za binadamu

23 Machi 2012

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa hakutakuwa na ulipizaji kisasi dhidi ya wale wanaopigania haki za binadamu nchini Sri Lanka kutokana na kutekelezwa kwa azimio na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu Sri Lanka.

Wanaharakati kutoka Sri Lanka waliosafiri kwenda Geneva wamekuwa wakipokea vitisho wakati unapoendelea mkutano wa baraza hilo mjini Geneva ukiwemo ujumbe wa watu 71 kutoka serikali ya Sri Lanka. Pia ripoti zinasema kuwa balozi wa Sri Lanka mjini Geneva amepokea barua ya vitisho ambayo kwa sasa inachunguzwa na polisi na idara ya ulinzi ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud