Ban akitaka Korea Kaskazini kutafakari upya uamuzi wa kuanzisha “satelite”

19 Machi 2012
 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka Jamhuri ya watu wa Korea kutafakari upya mpango wake wa uzinduzi  matumizi ya Satelite, akisema kuwa hatua hiyo lazima izingatie maazimio yaliyopitishwa na baraza la usalama.

Korea inakusudia kuzindua rasmi satelite mwezi ujao katika kile inachoeleza kuwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kiongozi wake hayati Kim Ii-sung.

Jumuiya ya kimataifa inaitaka Korea Kaskazini kusitisha jaribio lolote linaloweza kutafsiriwa kama njia ya kurusha angani luteka zake.                                                                                   

Ban amesema kuwa Korea inapaswa kufahamu kuwa jaribio lolote la kuweka makombora ya masafa ya mbali ni kwenda kinyume na azimio la baraza la usalama ambalo lilipiga marafuku majaribio kama hayo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter