Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU, UNiTE waadhimisha siku ya wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

AU, UNiTE waadhimisha siku ya wanawake kwa kupanda mlima Kilimanjaro

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake UNiTE wakishirikiana na makundi mengine ya kupigania haki za wanawake, Muungano wa Afrika na serikali ya Tanzania wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima Kilimanjaro.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hili kufanyika katika kuchagiza kupinga dhuluma dhidi ya wanawake na kushirikisha pia vijana kutoka sehemu mbalimbali kutoka barani Afrika wanaopiga debe kuulinda haki za wanawake.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa UNiTE John Hendra amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali za Afrika ikiwemo Tanzania katika kuboresha maendeleo ya wanawake.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)