Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Ivory Coast aridhishwa na uchaguzi mdogo nchini humo

Mwakilishi wa UM Ivory Coast aridhishwa na uchaguzi mdogo nchini humo

Mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI ameelezea kuridhishwa kwake na jinsi uchaguzi mdogo wa bunge ulivyoendeshwa nchini humo akisema upigaji kura umefanyika katika mazingira ya utulivu.

Bert Koenders ameyasema hayo katika mwisho wa ziara yake kwenye vituo mbalimbali vya uchaguzi, ziara ambayo aliambatana na maafisa mbalimbali wa kibalozi. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)