Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu wa UM aikaribisha ripoti ya Togo

Mkuu wa haki za binadamu wa UM aikaribisha ripoti ya Togo

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha kutolewa kwa ripoti na tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Togo kuhusu madai ya dhuluma za mateso yaliyotendwa kwa watu wanaoaminika kuhusika na mapinduzi ya mwaka 2009 nchini humo.

Ripoti hiyo iligundua kuwa wafungwa hao walidhulumiwa na ikataka hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika na kufanyiwa mabadiliko idara zilizohusika hasa shirika la ujasusi nchini humo. Pillay amesema kuwa serikali imejitolea katika kuyatekeleza mapendekezo ya ripoti hiyo na kufanya kila iwezalo kuhakikisha haki kwa waathiriwa na pia kuzuia vitendo kama hivyo siku za usoni .