Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yataka suluhu kwa wakorea wanaozuiliwa nchini China

UNHCR yataka suluhu kwa wakorea wanaozuiliwa nchini China

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaifuatilia kwa karibu hali ya watu 25 raia wa Korea Kaskazini waliokamatwa nchini China mwezi huu. UNHCR imekuwa ikiwasiliana na utawala nchini China kuhusu watu hao na kutaka pande zote zinazohusika kujaribu kupata suluhu litakalowahikikishia usalama wa watu hao. UNHCR imesema kuwa itatoa ushirikiano wake na kuendelea kushirikiana na pande zote kuhusu suala hili.