Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yasema kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Syria

Ripoti ya UM yasema kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Syria

Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliosambaa na unaoelekea kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu unatekelezwa nchini Syria kwa ufahamu na ridhaa ya uongozi wa ngazi ya juu wa taifa hilo.

Hii ni sehemu ya hitimisho la ripoti ya uchunguzi ya tume iliyoundwa na Umoja wa Mataifa kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)