Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Amerika Kusini zatakiwa kuboresha hali magerezani

Nchi za Amerika Kusini zatakiwa kuboresha hali magerezani

Nchi zilizo kwenye bara la Amerika kusini zimetakiwa kuboresha hali kwenye magereza yao na vituo vingine kufuatia kisa ambapo wafungwa waliangamia kwenye mkasa wa moto kwenye gereza moja nchini Honduras. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Matifa pia inasema kuwa kuna visa vingi vya ghasia ndani ya magereza suala ambalo inasema linachangiwa na misongamano magerezani.

Rubert Colvile kutoka kwa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anasema mataifa hayo yana wajibu wa kuhakikisha kuwa hali kwenye magereza sio ya kuwatesa wafungwa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)