UM waonya juu ya misongamano kwenye magereza barani Amerika Kusini

16 Februari 2012

Maafisa wanaohusuka na masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wamezitaka nchi za Amerika Kusini kutafuta suluhu la tatizo la misongamano kwenye magereza kufuatia mkasa ambapo mamia ya wafungwa waliangamia baada ya moto kuteketeza gereza moja nchini Honduras.

Zaidi ya wafungwa 300 waliripotiwa kuangamia kwenye mkasa huo uliotokea kaskazini mwa mji mkuu Tegucigalpa huku wengi wa wafungwa wakiwa hawajulikani waliko, na inahofiwa kuwa huenda wameangamia pia. Mshauri kuhusu masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa mataifa nchini Honduras aliiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa msongamano huenda ulichangia kuongezeka kwa idadi ya vifo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud