Mataifa yanayokua yashirikishwe kwenye uongozi wa dunia:Migiro

14 Februari 2012

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ametaka kujumuishwa kwa mataifa yanayokuwa kiuchumi kwenye uongozi wa dunia akisisitiza kwamba wanaotoa maamuzi hawazingatii mchango wa masoko mapya kwenye uchumi wa dunia. Akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuzinduliwa mpango wa maendeleo na demokrasia wa Helsinki Migiro amesema kuwa washika dau wote wanahitaji kushirikiana kwenye maendeleo ya dunia.

Bi Migiro ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unalenga katika kuhakikisha kuwa sera za ulimwengu zinazingatia mahitaji ya watu maskini na kusema kuwa njia bora ya kufanya hilo ni kupunguza mwanya kati ya watunza sera na watu wanaowakilisha.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter