Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washerehekea siku ya Radio Duniani

UM washerehekea siku ya Radio Duniani

Uwezo wa Radio wa kuwaunganisha watu na kuleta uelewano hii leo unasherehekewa kwenye siku ya kwanza kabisa ya kimataifa ya Radio. Tarehe 13 mwezi Februari ndiyo iliyotengwa na shirika la elimu, Sayansi na uatamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

Mkurugenzi wa shirika la UNESCO Irina Bokova amesema kwamba huku ulimwengu ukiendelea kushuhudia mabadiliko bado Radio kimeasalia chombo muhimu cha mawasiliano hasa kwenye sehemu za mbali vijini.

(SAUTI YA  IRINA BOKOVA)

Siku hii ya Radio duniani inahitimisha miaka 66 tangu kuanzishwa kwa Radio ya Umoja wa Mataifa