Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa uvumilivu kwa wanachama wa Baraza la Usalama la UM ulisabaisha kuvunjika kwa azimio kuhusu Syria

Ukosefu wa uvumilivu kwa wanachama wa Baraza la Usalama la UM ulisabaisha kuvunjika kwa azimio kuhusu Syria

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa ameelezea kujuta kwake baaada ya taifa lake kupinga azimio kuhusu Syria mwishoni mwa juma. Vitaly Churkin anasema kuwa nchi yake imesababisha madhara makubwa.

Amesema kuwa Baraza la Usalama lingeafikia makubaliano kama wenzake kutoka nchi za magharibi wangekuwa na uvumilivu. Amesema kuwa kinachofanyika nchini Syria ni kitu muhimu akiongeza kuwa kama wangefanya kazi siku mbili au tatu zaidi kungekuwa na azimio la kupitishwa.