Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa UM wataka hatua kuchukuliwa kuokoa uchumi wa dunia

Maafisa wa UM wataka hatua kuchukuliwa kuokoa uchumi wa dunia

Maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wameonya kwamba uchumi wa dunia kwa mara nyingine unaelekea pabaya. Katibu katika kitengo cha sera kwenye idara ya masuala ya uchumi na jamii kwenye Umoja wa Mataifa Robert Vos anasema kuwa dalili hizo tayari zimeanza kuonekana kwenye mataifa yaliyostawi.

Naye Rais wa baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa Milos Koterec ameonya kuwa kilichoanza kama msukosuko wa uchumi huenda ukaitumbukiza dunia kwenye hali mbaya ya uchumi kwa asillimia 1.2 chini kutoka 2010.