Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wauawa na wengine kukimbia kutokana na machafuko Moyale nchini Kenya

Watu wauawa na wengine kukimbia kutokana na machafuko Moyale nchini Kenya

Machafuko yanayoendelea kwenye wilaya ya Moyale nchini Kenya tangu Januari yameshakatili maisha ya watu 21, maelfu kukimbia nyumba zao na takribani 57,316 kutawanywa, wengi wao wakikimbia nchi jiraji ya Ethiopia kupata usalama.

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu nchini Kenya KRCS, mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo OCHA na vyombo vya habari. Kwa mujibu wa mashirika hayo watu wengine 48 waliuawa mwezi Oktoba mwaka jana. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)