Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa WFP akaribisha hukumu kwa watu waliouwa mfanyakazi wa shirika hilo

Mkurugenzi wa WFP akaribisha hukumu kwa watu waliouwa mfanyakazi wa shirika hilo

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Bi Josette Sheeran amekaribisha uamuuzi wa mahakama kuu ya Kenya kuwahukumu kwenda jela watu watano waliohusika na mauaji ya mfanyakazi wa shirika hilo Silence Chirara nchini Kenya mwaka 2008.

Watu hao watano wamehukumiwa kifungo cha miaka 56 kila mmoja. Bi Sheera amesema ingawa hakuna linaloweza kufanyika kumrejeshea uhai Chirara lakini haki na sheria vimechukua mkondo wake.Ameongeza kuwa hukumu hiyo inatuma ujumbe maalumu kwamba wale wote wanaowadhuru wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu watafikishwa mbele ya sheria.

Chirara aliyeacha mke na watoto wawili alikuwa raia wa Zimbabwe na aliuawa akiwa kazini akisaidia ugawaji wa chakula Sudan Kusini kama mkuu wa masuala ya kifundi kwenye mji wa Lokichoggio Kaskazini Magharibi mwa Kenya.