Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkuu wa kituo cha radio mjini Moghadishu

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkuu wa kituo cha radio mjini Moghadishu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amelaani vikali mauaji ya karibuni ya mkurugenzi wa kituo cha radio bwana Hassan Osman Abdi na ameutaka uongozi wa Somalia kuchunguza mauaji hayo na kuwafikisha wahusiaka kwenye mkono wa sheria.

Mahiga amesema amestushwa sana na mauaji hayo ya mmoja wa waandishi habari mahiri nchini Somalia. Abdi mwenye miaka 29 alikuwa mwandishi na mkurugenzi wa Radio Shabelle na aliawa kwa kpigwa risasi mjini Moghadishu Januari 28 mwaka huu. Mauaji yake pia yamelaaniwa vikali na mkrugenzi wa UNESCO Irina Bokova. Kutoka Nairobi Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)