UNESCO yaandaa kongamano kujadilia mauwaji ya Holocaust

31 Januari 2012

Wanahistoria pamoja na watafiti wanakutana hii leo Mjini Paris, Ufaransa katika kongamano la kimataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa lenye shabaha ya kuangazia athari za mauwaji ya Holocast ambazo kwa kiwango fulani zinaweza kuchochea mienendo ya kutovumiliana na kwenda kinyume na hulka mpya ya kibinadamu duniani kote. 

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO litatoa fursa kwa wajumbe kujadiliana juu ya umuhimu wa upashaji habari kuhusiana na matukio ya Holocaust katika mafungamano ya kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi.

 Pia litawapa nafasi wajumbe kujadilia umuhimu wa kuendelea kuhifadhi kumbukumbu ya Holocaust kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

 Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa uliadhimisha kumbukumbu ya waathirika wa mauwaji ya Holocaust ambayo huadhimishwa kila mwaka January 27.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter