Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ujumbe wa UM nchini Liberia anayeondoka aelezea umuhimu wa mapatano nchini humo

Mkuu wa ujumbe wa UM nchini Liberia anayeondoka aelezea umuhimu wa mapatano nchini humo

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia anayeondoka amesisitiza umuhimu wa kuwepo mapatano katika nchi hiyo akiongeza kuwa hiyo ni hatua muhimu ya kuhakikisha kuwa hatua zilizopigwa kufuatua uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika nchini humo mwaka uliopita zinaendelea.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL Margrethe Løj, amesema kuwa hiyo ni hatua kubwa inayoashiria maoni ya watu wa Liberia. Amesema kuwa ana uhakika kuwa Liberia itaendelea na wajibu wake katika kudumisha amani.