Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apanga kwenda Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuongeza msukumo mazungumzo ya amani

Ban apanga kwenda Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuongeza msukumo mazungumzo ya amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anategemea kuelekea Mashariki ya Kati ili kuzishawishi Israel na Palestina kujiingiza kwenye majadiliano ya usakaji amani.

Amesema ziara yake hiyo inayotazamia kuifanya wiki ijayo, inakuja katika wakati muhimu ambapo pande zote mbili zimeanza maandalizi ya kujerea kwenye majadiliano.

 Akizungumza na waandishi wa habari, Ban ametangaza kutembelea pia Jordan ambako amesema kuwa anazitia moyo pande zote kurejea kwa hiari kwenye meza ya majadiliano.

Mazungumzo ya moja kwa moja yalikwama kuendelea Septemba mwaka 2010 kufuatia hatua ya Israel kuendelea na ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la ukanda wa Gaza.